FOWADI wa Barcelona Lionel
Messi amesisitiza kuwa
hataondoka Klabuni hapo na
kwamba ripoti za kuwa yeye
alidai Kocha Luis Enrique
afukuzwe ni ‘uongo. ’
Hivi karibuni iliripotiwa kuwa
Messi, mwenye Miaka 27 ,
alitaka kuihama Barcelona
baada ya kugombana na Luis
Enrique.
Akiongea mara baada ya Jana
kuisaidia Barcelona
kuwachapa Mabingwa wa
Spain Atletico Madrid 3 -1
Uwanja Nou Camp katika Mechi
ya La Liga , Messi alitamka:
“ Sina nia ya kuhama na
kwenda Timu nyingine, si
Chelsea wala Manchester City.
Nimechoshwa na hivi vitu
vyote Watu wanavyosema
dhidi yangu. Sikuiomba Klabu
imfukuze Mtu yeyote!”
Messi amekuwa akiichezea
Barcelona tangu Mwaka 2004
alipoanza kuichezea Timu ya
Kwanza akitokea Chuo cha
Soka cha Klabu hiyo na kuweza
kutwaa Mataji na Tuzo kibao .
Baadhi ya Rekodi za Messi :
- Mfungaji Bora La Liga: Bao
258
- Mfungaji Bora Barcelona : 378
- Mfungaji Bora UEFA
Championz Ligi: 75
- Bao Nyingi Msimu mmoja wa
La Liga: 50
- Bao Nyingi kwa Msimu
mmoja : 73
- Kufunga Mabao kwa Mechi
mfululizo: Mechi 21
- Anaongoza kwa kutwaa Ballon
d 'Ors : Mara 4 .mpaka sasa
Messi aliongeza kusema:
" Watu wanadhani mimi ndio
naendesha Klabu na hivyo
sivyo . Simwambii Mtu yeyote
kufanya uamuzi .
Kila
kinachosemwa ni uongo na
nataka Watu wajue kwamba
kila kitu ni uongo. Watu
wanasema haya kwa sababu
wanataka kutudhuru . Inaumiza
kwa sababu haya yamesemwa
na Watu wa Barca. Lazima
tuungane !”
Kufunguka kwa Messi
kunahitimisha Wiki ngumu kwa
Barca hasa baada ya uvumi
huo wa ugomvi na Luis Enrique
na yeye kudaiwa kuhama na
kisha pale Rais wa Klabu hiyo,
Josep Maria Bartomeu,
alipotangaza kufanyika
Uchaguzi wa Rais mwishoni
mwa Msimu huu badala ya
Mwakani ili kuondoa
mgawanyiko ndani ya Klabu.