Social Icons

Pages

Tuesday, 26 August 2014

YANGA YAWAZIDI MAPATO SIMBA HUKO ZANZIBAR



KWA HABARI ZAIDI.....
Yanga imeingiza mapato mengi zaidi katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya Shangani iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kushinda kwa mabao 2-0, mapato yaliyopatikana ni Sh milioni 7 na ushee.
Lakini wapinzani wake Simba wameingiza Sh milioni 3 tu katika mechi yao ya kirafiki iliyopigwa jana hiyo na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kilimani.
Yanga ndiyo ilianza kucheza halafu mashabiki wote wakatolewa nje na kuanza kuingia upya kushuhudia mechi ya pili ambayo ilikuwa ya Simba.
Ingawa mapato hayo yamekuwa yakifanywa siri kubwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), lakini   Yanga wameingiza mapato mengi zaidi.
Kiingilio katika mechi hizo ilikuwa ni Sh 2,000  na 5,000.
 
FULU VIWANJA