Social Icons

Pages

Sunday, 2 February 2014

LA LIGA: ATLETICO YAONGOZA, REAL YABANWA, RONALDO NYEKUNDU!


ATLETICO MADRID ndio Vinara wapya wa La Liga baada kuichapa Real Sociedad Bao 4-0 huku Real Madrid wakitoka Sare na Athletic Bilbao na Cristiano Ronaldo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu ya utata.
Atletico walifunga Bao zao kupitia David Villa, Diego Costa, Miranda na Diego Ribas.
Ushindi huo umeifanya Atletico iongoze Ligi kwa mara ya kwanza tangu 1996 na wapo Pointi 3 mbele ya Barcelona na Real Madrid ambao wamefungana kwa Pointi.

MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Atletico de Madrid
22
18
3
1
56
14
42
57
2
FC Barcelona
22
17
3
2
59
16
43
54
3
Real Madrid CF
22
17
3
2
61
22
39
54
4
Athletic de Bilbao
22
13
4
5
42
28
14
43

ATLETICO-COPA_DEL_REYNao Real Madrid, wakicheza Ugenini, walishindwa kuipiku Barca na kukamata Nafasi ya Pili baada kutoka Sare 1-1 na Athletic Bilbao.
Real walitangulia kufunga kwa Bao la Jese Rodriguez katika Dakika ya 64 na Bilbao kusawazisha kupitia Ibai Gomez Dakika 10 baadae.
Ndipo ilipotokea rabsha Golini na Ronaldo kupewa Kadi Nyekundu wakati marudio yalionyesha hakufanya kosa lililostahili Kadi hiyo.

 
FULU VIWANJA