!
JUMATATU
Usiku, Etihad, itazikutanisha Manchester City na Chelsea ambazo
zinaifukuza Arsenal iliyo kileleni mwa Ligi Kuu England na umuhimu wa
Mechi hii haujapotea kwa Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, ambae Siku
zote yuko tayari kutumia mbinu yeyote ili kuzua hofu na kuwapoteza
Wapinzani wake.
Safari hii, Mourinho ameipania Man City,
ambao pamoja na Arsenal, ndio wanaonekana ni tishio kwake katika mbio
za Ubingwa Msimu huu.
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
|
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
|
1 |
Arsenal |
24 |
26 |
55 |
|
2 |
Man City |
23 |
42 |
53 |
|
3 |
Chelsea |
23 |
23 |
50 |
|
4 |
Liverpool |
24 |
29 |
47 |
|
5 |
Everton |
24 |
12 |
45 |
|
6 |
Tottenham |
24 |
-1 |
44 |
|
7 |
Man Utd |
24 |
10 |
40 |
+++++++++++++++++++++++++++
Akiongea na Wanahabari kuelekea mpambano
wao muhimu, Mourinho aliiponda Man City na kudai haijafanya lolote la
maana tangu inunuliwe na Tajiri toka Falme za Nchi za Kiarabu, Sheikh
Mansour, Mwaka 2008 ukilinganisha na Fedha alizotumia.
Tangu wakati huo, Man City imetwaa FA
CUP Mwaka 2011, Ligi Kuu England Mwaka 2012 lakini kwenye UEFA CHAMPIONZ
LIGI ni Msimu huu tu wamefika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada ya
kutupwa nje mara mbili kwenye Hatua za Makundi na hata safari hii wana
kimbembe kwani Mpinzani wao ni Barcelona ambae watacheza nae Mechi ya
Kwanza Etihad Februari 18.
Mourinho amesema: “Wametwaa Ubingwa mara moja, Vikombe viwili. Timu yao nzuri na wanatakiwa kushinda Mataji mengi zaidi!”
Wamiliki hao wa Man City, tangu Mwaka 2008 wametumia zaidi ya Pauni Milioni 700 kununua Wachezaji.
Lakini Mourinho amepinga kauli ya Meneja
wa Tottenham, Tim Sherwood, ambae alidai Man City ndio Timu Bora
Duniani mara baada ya Juzi kutwangwa Bao 5-1 na City, Spurs walipokuwa
Uwanjani kwao White Hart Lane.
Mourinho amedai City wana bahati na pia kusaidiwa na Marefa.
+++++++++++++++++++++++++++
Man City==Bahati yao ya Mtende:
26 Desemba: Ushindi wao 2-1 na Liverpool
- Raheem Sterling alifunga Bao safi kuipa uongozi Liverpool na Refa akaamua Ofsaidi
- Luis Suarez alivutwa Jezi waziwazi na Joleon Lescott Dakika za mwishoni na Refa kupeta.
12 January: Ushindi wao 2-0 na Newcastle
- Cheick Tiote alifyatua mzinga wa Mita
25 na kutinga wavuni lakini Refa akaamua Yoan Gouffran alikuwa Ofsaidi
licha ya kutohusika chochote.
29 January: Ushindi wao 5-1 na Tottenham
- Wakiwa nyuma kwa Bao 1-0, Spurs walisawazisha kwa Bao safi la Michael Dawson lakini likakataliwa kwa Ofsaidi.
- Danny Rose, Beki wa Spurs, alitolewa
nje kwa Kadi Nyekundu licha ya kuucheza Mpira ikidaiwa alimchezea Rafu
Edin Dzeko na kutolewa Penati iliyowapa City Bao la pili na kuongoza
2-0.
Akipasua ukweli wake, Mourinho ametamka:
“Maumuzi mengi muhimu yamekwenda upande wao. Wana bahati. Marefa
wanajitahidi na na mara nyingne wanafanya makosa na kawaida makosa hayo
hugawanyika kwa kila Timu. Lakini kwao, kila kitu kipo upande wao.”
Hata hivyo, Meneja wa Man City, Manuel
Pellegrini, alikataa kuvutwa katika mzozo na Mourinho na kudai: “Hii si
Mimi dhidi ya Mourinho au yeye na Mimi! Jumatatu ni Manchester City
dhidi ya Chelsea, Timu zote zinagombea Ubingwa.”
Kwenye Mechi hii, Man City itamkosa
Straika wao mahiri Sergio Aguero, ambae Msimu huu ameshafunga Bao 26,
alieumia Musuli ya Pajani [Hamstring] walipoifunga Tottenham.
Man City wameshinda Mechi zao zote 11 za
Ligi walizocheza Uwanjani kwao Etihad Msimu huu wakipiga wastani wa Bao
4 kila Mechi na tayari washabamiza Jumla ya Mabao 115 katika Mechi zao
zote za Msimu huu.