Thursday, 19 December 2013
YANGA SC WAINGIA KAMBINI PROTEA BILA OKWI
YANGA
SC wameingia kambini jioni hii katika hoteli ya Protea, Dar es Salaam
kujiandaa na mpambano dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC wa Nani
Mtani Jembe, lakini mshambuliaji mpya Emmanuel Arnold Okwi bado
hajawasili.
Baadhi
ya wapenzi wa Yanga na Waandishi wa Habari walifika Uwanja Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kumpokea Okwi, lakini
hakutokea na hakukuwa na taarifa za kutokea hadi wakaondoka.
Lakini
kocha Mholanzi, Ernie Brandts ameingia kambini jioni hii na wachezaji
wake wote wengine kujiandaa na mchezo wa Jumamosi unaoandaliwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wadhamini wa Simba na Yanga.
Viingilio
vya mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu Sh.
7,000, rangi ya chungwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000
wakati VIP A Sh. 40,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja katika vituo mbalimbali, mchezo huo
utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Vituo
ambavyo tiketi hizo zitauzwa kesho (Ijumaa) ni Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala,
Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi
hiyo itachezeshwa na Ramadhan Ibada (Kibo) kutoka Zanzibar,
atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba, na Simon Charles kutoka
Dodoma. Mwamuzi wa akiba ni Israel Nkongo wa Dar es Salaam wakati
mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha.