Social Icons

Pages

Wednesday, 18 December 2013

MAN UNITED WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA LIGI, SPURS NJE

KOCHA David Moyes ameendelea kupambana baada ya jana kuiongoza Manchester United kushinda mabao 2-0 dhidi ya Stoke City katika Kombe la Ligi England.
Ushindi huo wa United jana ulitokana na mabao ya Ashley Young dakika ya 61 na Patrice Evra dakika ya 78. 
Raha ya bao: Ashley Young (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dhidi ya Stoke City

Katika mchezo mwingine, mshambuliaji Emmanuel Adebayor alirejea uwanjani na kufunga bao moja wakati timu yake, Tottenham Hotspur ikifungwa 2-1 na West Ham United, mabao ya 
Jarvis dakika ya 80 na Maiga dakika ya 85.
Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City. 
Adebayor akishangilia bao lake ambalo hata hivyo halikuweza kuinusuru Spurs na kipigo www.fulu viwanja blogspot.com
 
FULU VIWANJA