Social Icons

Pages

Thursday, 19 December 2013

WACHEZAJI RAJA CASABLANCA WAGOMBEA VIATU VYA RONALDINHO...NI MARA TU BAADA YA WAMOROCO HAO KUIFUNGA TIMU YAKE 3-1 KOMBE LA DUNIA

MARA tu baada ya kutolewa katika Klabu Bingwa ya Dunia a FIFA, wazi Ronaldinho alitaka kurejea chumba cha kubadilishia nguo cha Atletico Mineiro kujiliwaza.
Lakini alilazimika kubaki uwanjani baada ya kuvamiwa na wachezaji wa Raja Casablanca, waliomsalimia na kumuomba viatu vyake vya Nike!
Timu hiyo Morocco iliendeleza wimbi lake la ushindi nyumbani kwa ushindi wa mabao 3-1, wakimtoa nishai Mbrazil huyo ambaye alifunga bao zuri la mpira wa adhabu- katika jitihada zake za kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu alipofika fainali akiwa na Barcelona mwaka 2006.
Kitimutimu: Wachezaji wa Raja Casablanca wakiwa wamemzunguka Ronaldinho kugombea viatu vyake

The lucky man: Vivien Mabide with one of the boots after the game
Mwenye bahati yake: Vivien Mabide akiwa ameshika moja ya viatu hivyo baada ya mechi
Dancing feet: Never mind the shock win, Casablanca players got their precious souvenirs, too
Wachezaji wa Casablanca 

Mouchine aliifungia Raja bao la kwanza kabla ya Ronaldinho kusawazisha. Lakini Raja ikapata bao la pili dakika ya 84 kwa penalti na Vivien Madibe akahitimisha ushindi huo dakika ya mwisho kwa bao la tatu.
Timu hiyo ya Morocco sasa itamenyana na mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich Jumamosi katika Fainali mjini Marakech.
 
FULU VIWANJA