skip to main |
skip to sidebar
OKWI NIKIPATA NAFASI NITACHEZA KAMA MCHEZAJI WA KIMATAIFA
MSHAMBULIAJI
mpya wa Yanga SC, Emmanuel Arnold Okwi amesema japokuwa hajapata fursa
ya kufanya mazoezi na timu yake mpya, lakini hana wasiwasi akipangwa kesho
Jumamosi katika mechi dhidi ya timu yake zamani, Simba SC atacheza kwa
uelewano mzuri na wachezaji wenzake wapya, kwa kuwa yeye ni mchezaji wa
kimataifa.
Okwi
aliyewasili jana Dar es Salaam akitokea kwao, kampala, Uganda kuja
kuanza kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili, aliiambia BIN ZUBEIRY
jana kwamba hana shaka akipangwa atacheza vizuri na kuwafurahisha
mashabiki wa timu yake hiyo mpya kwa sababu ana uzoefu wa kimataifa.
“Kwanza
mtu kama (Mrisho) Ngassa nimecheza naye Simba SC, na (Hamisi) Kiiza
tunacheza naye timu ya taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa
nao tutacheza kwa uelewano sana pale mbele na nitafunga,”alisema Okwi.
Lakini
Okwi amesema kwa ujumla anaijua Yanga vizuri na anajua uchezaji wa
wachezaji wake wengi, hivyo anaweza kucheza vizuri katika mfumo wa timu.
“Unaweza
kuitwa timu ya taifa, siku mbili kabla ya mechi na wakati mwingine
unakuta wachezaji wengi hujawahi kucheza nao kabisa, lakini mnafanya
mazoezi siku moja mnaelewana na mnacheza vizuri,”alisema Okwi.
Simba
na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo,
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Katika
mchezo huo, utakaochezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka
Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles
kutoka Dodoma, iwapo dakika 90 zitaisha kwa sare, sheria ya mikwaju ya
penalti itatumika kuamua mshindi.
Viingilio
vya mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu Sh.
7,000, rangi ya chungwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000
wakati VIP A Sh. 40,000 na tiketi za mchezo huo utakaoanza Saa 10:00
jioni zitaanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali.
Vituo
hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa
Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza
Madukani.
Wachezaji
wanaoruhusiwa kucheza mechi ya kesho ni wale waliosajiliwa ama kikosi
cha kwanza au timu ya vijana pamoja na wapya ambao wameombewa usajili
katika dirisha dogo