
Inadaiwa kuwa Vincent Tan, Raia wa Malaysia, alituma Barua pepe ikimtaka Malky Mackay, Miaka 41, ajiuzulu ama afukuzwe kazi.
Hali tete imeikumba Cardiff City tangu
Mwezi Oktoba wakati Tan alipomtimua Mkuu wa Usakaji Vipaji na Usajili
Wachezaji, Iain Moody, ambae alikuwa na uzoefu mkubwa na kumweka Kijana
mdogo wa Miaka 23 kwenye nafasi hiyo.
Hali ilizidi kuchafuka Klabuni hapo
wakati Mtendaji Mkuu wake, Simon Lim, alipotoa Taarifa Siku ya Jumatatu
kwamba Tan amekasirishwa sana na matakwa ya Malky Mackay ya kutaka
Wachezaji wengine Mwezi Januari wakati mwanzoni mwa Msimu alitumia Pauni
Milioni 50 kununua Wachezaji.
Lim aliongeza kuwa Mackay hatapewa hata Senti moja kuongeza Wachezaji hiyo Januari.
Licha ya kusakamwa, Mackay, ambae
Mkataba wake unamalizika Mwaka 2016, amegoma kujiuzulu na anaendelea na
kazi yake na leo anatarajiwa kuongea na Wanahabari katika Mahojiano ya
kawaida kabla ya Mechi yao ya Jumamosi ambayo watasafiri kwenda Anfield
kucheza na Liverpool.
Nae Brendan Rodgers, Meneja wa
Liverpool, ambae ni Rafiki wa karibu wa Mackay, amemshambulia Vincent
Tan kwa kumdhalilisha Rafiki yake na kumwambia Raia huyo wa Malaysia
‘hajui lolote kuhusu Soka!’
Hadi sasa kwenye Ligi Kuu England, baada
ya Mechi 16, Cardiff City wapo Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 4 juu ya zile
Timu 3 za mkiani ambalo ndio eneo la kushushwa Daraja.