Social Icons

Pages

Friday, 20 December 2013

COLE KUENDELEA KUSOTA BENCHI CHELSEA IKICHEZA NA ARSENAL

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amekataa kumlaumu Ashley Cole kwa kuhudhuria Pati ya Krismasi ya Arsenal lakini amethibitisha Beki huyo hana Namba wakati Chelsea itakapokwenda Emirates kucheza na Arsenal Jumatatu kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Cole, Miaka 33, alipigwa Picha akiwa kwenye Pati ya Arsenal Jumatano ikiwa ni Siku moja tu tokea Chelsea ifungwe na Sunderland na kutupwa nje ya Capital One Cup.
Mourinho amesema: “Naweka maoni yangu kwangu mwenyewe-ilikuwa ni Siku ya Ofu kwa Wachezaji. Mimi sio Baba, ni Meneja.”
Aliongeza: “Tangu mwanzo, Ashley alikuwa hachezi. Lakini leo ni Ijumaa, Gemu ipo Jumatatu. Kunaweza kutokea kitu. Ila nishaamua Branislav Ivanovic ni Fulbeki wa Kulia, nitamchezesha Cesar Azpilicueta Fulbeki kushoto, nitamchezesha John Terry na inabidi niamue kati ya Gary Cahill na David Luiz.”
Cole, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa England, alicheza Siku ya Jumanne wakati Chelsea inafungwa 2-1 na Sunderland na kutupwa nje ya Capital One Cup lakini katika Wiki za hivi karibuni Namba yake imechukuliwa na Cesar Azpilicueta na hajacheza kwenye Ligi tangu Chelsea ifungwe 2-0 na Newcastle hapo Novemba 2
 
FULU VIWANJA