COPA
del REY, Kombe la Mfalme huko Spain, leo lipo kwenye Mechi za Marudiano
za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na Mabingwa wa Spain, Barcelona wako
kwao Nou Camp kurudiana na Timu ya Daraja la chini, FC Cartagena, ambayo
waliitwanga 4-1 Wiki mbili zilizopita.
Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey,
Atletico Madrid, wako kwao Estadio Vicente Calderon, kurudiana na Sant
Andreu, pia ya Daraja la chini, ambayo waliifunga 4-0.
Lakini, macho yote yatakuwa huko
Santiago Bernabeu, ambako Vigogo, Real Madrid, wanarudiana na Timu
ndogo, Olimpic Xativa, waliyotoka nayo 0-0 katika Mechi ya Kwanza ambayo
walicheza bila Cristiano Ronaldo aliekuwa Kifungoni kufuatia Kadi
Nyekundu aliyopewa kwenye Fainali ya Kombe hili Msimu uliopita Real
walipofungwa 2-1 na Atletico Madrid.