KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya michezo.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 17 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana
Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika
kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya
kikanda na kimataifa.
“Airtel
Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya
miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
“Tutaendelea
kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi
inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa”
alisema
Colaso
alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising
Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana
wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.
Wakati
wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United Andy Cole aliwaasa
vijana hao chini ya miaka 17 kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za
kucheza kwenye timu kubwa duniani.
“Nimeona
vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa
kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi
kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya
uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio”
Alisema.
Nae
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliwashukuru kampuni ya Airtel
Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa
makapuni mengine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo
“Tunahitaji
nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka
maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika
michezo, niwaombe makampuni mengine waige mfano huu katika kusaidia
juhudi za Serikali kuendeleza michezo.