Social Icons

Pages

Saturday, 26 March 2016

MESSI ASEMA NAYE ATAFURAHIA SANA AKIPATA NAFASI YA KUKUTANA NA OBAMA


Baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama kusema mabinti zake Malia na Sasha wamekuwa wakitaka kukutana na Lionel Messi, mshambuliaji huyo wa Barcelona, naye amejibu.

Messi amesema naye angefurahi zaidi kukutana na Obama kwa kuwa ni kati ya watu ambao amekuwa na ndoto ya kukutana nao ana kwa ana.

Wiki iliyopita, Obama alisema wanaye wanapenda soka na hasa wamekuwa wakivutiwa zaidi na mshambuliaji huyo raia wa Argentina lakini hakuwa amepata nafasi ya kuandaa jambo hilo.





 
FULU VIWANJA