Social Icons

Pages

Tuesday, 22 March 2016

LUIS SUAREZ AREJEA URUGUAY KWA MARA YA KWANZA KUIVAA BRAZIL TANGU KIFUNGO KUNG'ATA MENO!

STRAIKA mahiri wa FC Barcelona Luis Suarez amerejea kwenye Timu ya Taifa ya Uruguay kwa mara ya kwanza tangu amalize Kifungo chake cha kumng'ata Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
SUAREZ-AREJEA-URUGUAY

Kifungo cha Suarez kilikuwa ni cha Miezi Minne kutojihusisha na kitu chochote kwenye Soka, ambacho alikimaliza Oktoba 2014, Faini na pia kufungiwa Mechi 9 kutoichezea Uruguay.

Juzi Jumatatu, Suarez alijumuika kambini kwenye Timu ya Taifa ya Uruguay huko Montevidio, Uruguay ikiwa ni mara ya kwanza tangu 2014.
Uruguay itapambana na Brazil huko Recife, Brazil na Jumatano ijayo kuivaa Peru nyumbani kwao zikiwa ni Mechi za Mchujo za Kanda ya Marekani ya Kusini za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
Ratiba:
**Saa za Bongo
Alhamisi Machi 24         
23:00 Bolivia v Colombia  
24:00 Ecuador v Paraguay
03:30 Chile v Argentina    
Ijumaa Machi 25
05:15 Peru v Venezuela    
Jumamosi Machi 26
03:45 Brazil v Uruguay     
Jumanne Machi 29
23:30 Colombia v Ecuador
24:00 Argentina v Bolivia 
24:00 Paraguay v Brazil   
24:00 Venezuela v Chile   
24:00 Uruguay v Peru
 
FULU VIWANJA