
Akizungumza kutok mjini Addis Ababa leo, Kapombe anayechezea Azam FC amesema kwamba kucheza Ulaya ni ndoto ya kila mchezaji wa Afrika.
“Watu walinilaumu sana mwaka juzi nilipoondoka AS Cannes (ya Ufaransa) kuja Azam, lakini hawakujua tu. Ni mambo mengi ambayo siwezi kusema,”amesema Kapombe.
Hata hivyo, beki huyo wa zamani wa Simba amesema alichojifunza ni kwamba hatakubali ofa yoyote ya kwenda Ulaya kujiunga na timu ya chini ya Daraja la Kwanza.
“Mimi ni mchezaji wa kimataifa, nina nafasi timu yangu ya taifa na klabu yangu inacheza mashindano makubwa, nina uzoefu wa kutosha kucheza popote,”amesema na kuongeza; “Wakala anayetaka kunipa dili la Ulaya, basi liwe la klabu ya Daraja la kwanza, au Ligi Kuu,”amesema.Pamoja na hayo, Kapombe amesema hawezi kuondoka Azam FC kujiunga na klabu nyingine yoyote Tanzania.