Social Icons

Pages

Wednesday, 26 August 2015

CAPITAL ONE CUP YALETA DABI KADHAA!

Image result for image of capital one league

Droo ya Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, Capital One Cup kama linavyojulikana, limezaa Dabi safi kadhaa baada ya kufanywa Jana.
Tottenham, ambao Mwaka 2008 walitwaa Kombe hili huku njiani wakiitwanga Arsenal 5-1 katika Mechi mbili, wataivaa Arsenal Uwanjani White Hart Lane katika Dabi ya London ya Kaskazini.
Dabi nyingine ni ile ya Jiji la Birmingham itakayochezwa Villa Park kati ya Aston Villa na Birmingham.
Mabingwa Watetezi wa Capital One Cup, Chelsea, wao wamepangiwa kucheza Ugenini na Timu ndogo Walsall.
Dabi nyingine ni ile ya Timu za London Uwanjani Selhurst Park kati ya wenyeji Crystal Palace na Charlton Athletic.
Nao Sunderland wataikaribisha Man City wakati Man United wapo kwao Old Trafford kucheza na Timu ya Daraja la Championship Ipswich Town.
Mechi nyingine mbili za Klabu za Ligi Kuu England pekee ni zile za Leicester City na West Ham wakati Norwich City wakicheza na West Bromwich Albion.
Klabu nyingine za Ligi Kuu England ambazo bado zipo Mashindanoni baada ya Mechi za Raundi ya Pili zitacheza Ugenini wakati Fulham ikiivaa Stoke City, Hull City na Swansea City na MK Dons wakiikwaa Southampton huku Everton wakiwa Wageni wa Barnsley.
Mechi zote hizi zitachezwa Wiki ya kuanzia Septemba 21.
DROO KAMILI:
Man United v Ipswich Town
Liverpool v Carlisle
Crystal Palace v Charlton
Middlesbrough v Wolves
Norwich v West Brom
Hull v Swansea
Leicester v West Ham
Aston Villa v Birmingham
Tottenham v Arsenal
Sunderland v Man City
Newcastle v Sheffield Wednesday
Reading v Barnsley/Everton
Preston v Bournemouth
Walsall v Chelsea
MK Dons v Southampton
Fulham v Stoke City
 
FULU VIWANJA