MECHI 4 ZA LIGI KUU ENGLAND ZILIZOANA SAA 11 JIONI:
Bournemouth 0 Aston Villa 1
Bournemouth wameanza kampeni yao ya kwanza kabisa katika Historia yao ya kucheza Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Aston Villa.
Hadi Mapumziko, Gemu ilikuwa 0-0.
Bao la ushindi kwa Villa lilifungwa na Mchezaji wao mpya Rudy Gestede alietokea Benchi na kupachika wavuni katika Dakika ya 72.
Ijumaa Aston Villa watakuwa kwao Villa Park kucheza na Manchester United.
Matchday 1
VIKOSI:
Bournemouth: Boruc, Francis, Elphick, Cook, Daniels, Ritchie, Gosling, Surman, Pugh, King, Wilson.
Akiba: Gradel, Mings, Smith, Kermorgant, Federici, Distin, O’Kane.
Aston Villa: Guzan, Bacuna, Richards, Clark, Amavi, Veretout, Gueye, Westwood, Sinclair, Ayew, Agbonlahor.
Akiba: Baker, Cole, Richardson, Hutton, Sanchez, Bunn, Gestede.
REFA: Mark Clattenburg
Norwich 1 Crystal Palace 3
Wenyeji Norwich walijikuta wakienda Haftaimu wakiwa Bao 1 nyuma ya Crystal Palace ambao walifunga katika Dakika ya 40 kwa Bao la Wilfried Zaha.
Kipindi cha Pili Damien Delaney aliipa Palace Bao la pili na Nathan Redmond kuifungia Norwicha Bao lao moja lakini Mchezaji mpya Yohan Cabaye akapiga Bao la 3 katika Dakika za Majeruhi na kuipa Palace ushindi wa 3-1.
VIKOSI:
Norwich: Ruddy, Whittaker, Martin, Bassong, Brady, Howson, Johnson, Tettey, Hoolahan, Dorrans, Grabban.
Akiba: Wisdom, Jerome, Hooper, Rudd, Redmond, Ryan Bennett, O’Neil.
Crystal Palace: Alex McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Mutch, Cabaye, McArthur, Zaha, Puncheon, Murray.
Akiba: Bamford, Bolasie, Hennessey, Jedinak, Gayle, Wickham, Kelly.
REFA: Simon Hooper
Everton 2 Watford 2
Everton, wakicheza kwao Goodison Park, wametoka Sare 2-2 na Watford iliyopanda Daraja Msimu huu.
Katika Dakika ya 14, Miguel Layun aliipa Bao Watford ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
Ross Barkley akaisawazishia Everton katika Dakika ya 76 lakini Odion Ighalo akaipeleka tena Watford kwa Bao la Dakika ya 83.
Lakini Dakika 3 baadae Kone alietokea Benchi alifunga Bao kwa Everton na Mechi kwisha 2-2.
VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Stones, Galloway, Cleverley, McCarthy, Barry, Mirallas, Barkley, Lukaku.
Akiba: Robles, Oviedo, Kone, Naismith, Osman, Browning, McAleny.
Watford: Gomes, Nyom, Cathcart, Prodl, Holebas, Layun, Capoue, Behrami, Anya, Jurado, Deeney.
Akiba: Angella, Vydra, Gilmartin, Paredes, Pudil, Watson, Ighalo.
REFA: Mike Jones
Leicester 4 Sunderland 2
Leicester City wakicheza kwao chini ya Meneja wao mpya Claudio Ranieri wameichapa Sunderland Bao 4-2.
Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy la Dakika ya 11 na Riyad Mahrez kuongeza Bao la Pili katika Dakika ya 18 na pia la tatu kwa Penati ya Dakika ya 25.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Lee Catermole kumchezea rafu Riyad Mahrez.
Hadi Mapumziko, Leicester 3 Sunderland 0.
Kipindi cha Pili Sunderland walipata Bao moja kupitia Jermaine Defoe lakini Leicester wakapiga Bao la 4 lilofungwa na Marc Albrighton wakati Steven Fletcher aliipa Sunderland Bao lao la pili na Mechi kwisha 4-2.
VIKOSI:
Leicester: Schmeichel, De Laet, Huth, Morgan, Schlupp, Albrighton, Drinkwater, King, Mahrez, Okazaki, Vardy.
Akiba: Hammond, Kante, Kramaric, Ulloa, Fuchs, Benalouane, Schwarzer.
Sunderland: Pantilimon, Jones, Coates, Kaboul, Van Aanholt, Cattermole, Johnson, Rodwell, Larsson, Lens, Defoe.
Akiba: Bridcutt, Matthews, O’Shea, Graham, Giaccherini, Mannone, Fletcher.
REFA: Lee Mason
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Agosti 8
Man United 1 Tottenham 0
Bournemouth 0 Aston Villa 1
Everton 2 Watford 2
Leicester 4 Sunderland 2
Norwich 1 Crystal Palace 3
1930 Chelsea v Swansea City
Jumapili Agosti 9
1530 Arsenal v West Ham
1530 Newcastle v Southampton
1800 Stoke v Liverpool
Jumatatu Agosti 10
2200 West Brom v Man City
Ijumaa Agosti 14
2245 Aston Villa v Man United