LIGI KUU ENGLAND: MABINGWA CHELSEA WANASA, KIPA WAO ALA NYEKUNDU!
- Mabingwa Watetezi wameanza vibaya kampeni yao ya kutetea Taji lao baada ya kutoka Sare 2-2 na Swansea City Uwanjani
Stamford kwenye Mechi ambayo walicheza Mtu 10 kwa zaidi ya Nusu Saa baada Kipa wao Thibaut Courtois kupewa Kadi Nyekundu.

Chelsea walitangulia kufunga kwa frikiki ya Oscar lakini Mchezaji mpya wa Swansea anaetoka Ghana, Andre Ayew, aksawazisha.
Federico Fernandez wa Swansea alijifunga mwenyewe akijaribu kuokoa krosi ya Willian na kuipa Chelsea uongozi wa 2-1.
MAGOLI:
Chelsea 2
-Oscar Dakika ya 23
-Fernandez 30 (Kajifunga mwenyewe)
Swansea 2-Andre Ayew Dakika ya 29
-Gomis 55 (Penati)
Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois alitoa Penati katika Dakika ya 51 alipomchezea rafu Bafétimbi Gomis na kupewa Kadi Nyekundu na Chelsea kulazimika kumtoa Oscar ili Kipa akiba Asmir Begovic aingie.
Bafetimbi Gomes akamchambua Kipa Begovic na kufunga Bao ambalo limeipa Sare ya 2-2.