Social Icons

Pages

Saturday, 8 August 2015

LIGI KUU ENGLAND: MAN UNITED WAANZA NA USHINDI!

LIGI KUU ENGLAND: MAN UNITED WAANZA NA USHINDI!

LIGI KUU ENGLAND Leo imeanza rasmi Msimu wake mpya wa 2015/16 huko Old Trafford Jijini Manchester na Wenyeji Manchester United kuibuka na ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Tottenham Hotspur.
Man United hii Leo iliwatumia Wachezaji wake wanne wapya kuanza Mechi hii ambao ni Kipa Sergio Romero, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay na kisha walimuingiza Bastian Schweinsteiger kumbadili Michael Carrick.Manchester United 1-0 Tottenham: Walker own goal gets Van Gaal off to a winning start
Dakika ya 22 Beki wa Spurs Kyle Walker alijifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa wakati Kepteni Wayne Rooney akijiandaa kupiga na kuipa Man United uongozi wa Bao 1-0.
Bao hilo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.
Mechi inayofuata ya Ligi kwa Man United ni Ijumaa ijayo Ugenini Villa Park watakapocheza na Aston Villa.
Baadae Leo zitachezwa Mechi nyingine 5 za Ligi Kuu England.
 
FULU VIWANJA