Social Icons

Pages

Wednesday, 26 August 2015

BALOTELLI ATIMKA LIVERPOOL! CUADRADO ANG’OKA CHELSEA, STONES NA CHELSEA, SHIDA! BERAHINO AGOMEWA!

JUAN CUADRADO AONDOKA CHELSEA!

Mchezaji wa Chelsea Juan Cuadrado ametua kwa Mabingwa wa Italy Juventus kwa Mkopo wa Msimu mmoja ikiwa ni Miezi 7 tu tangu Mabingwa hao wa England wamnunue.
Cuadrado, Raia wa Colombia mwenye Miaka 27, alijiunga na Chelsea kutoka Fiorentina Februari Mwaka huu kwa Dau la Pauni Milioni 23.3 lakini amecheza 15 tu na kati ya hizo ameanza 4 tu.Image result for image MARIO BALOTELLI,Juan Cuadrado
Kuondoka kwa Cuadrado kunafuatia Chelsea kumsaini Winga wa Barcelona Pedro Alhamisi iliyopita.
MARIO BALOTELLI AONDOKA LIVERPOOL!
Straika wa Liverpool Mario Balotelli amemaliza upimwaji afya yake huko Italy Klabuni AC Milan akiwa njiani kusaini Mkataba wa Mwaka mmoja wa Mkopo.Image result for image MARIO BALOTELLI,Juan Cuadrado
Ili kukamilisha Uhamisho huu, Balotelli alilazimika kukubali kupunguzwa Mshahara huku baadhi ya huo Mshahara ukilipwa na Liverpool wakati akiwa huko kwao Italy.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Straika huyo wa Italy mwenye Miaka 25 kuichezea AC Milan na mwenyewe amekiri Klabu hiyo iko moyoni mwake.Image result for image MARIO BALOTELLI,Juan Cuadrado
Balotelli alihamia Liverpool Agosti 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 16 lakini ameifungia Bao 1 tu kwenye Ligi Kuu England.
Kwa Msimu huu mpya, Liverpool imewasaini Mafowadi Christian Benteke, Roberto Firmino na Danny Ings, na pia Divock Origi amerejea Anfield baada ya kuwa kwa Mkopo huko Ufaransa Klabuni Lille tangu anunuliwe huko huko Mwaka Jana
SAIDO BERAHINO-WBA WAIGOMEA OFA!
West Bromwich Albion wameikataa Ofa ya pili ya Tottenham Hotspur ya kumnunua Straika wao Saido Berahino.
Wiki iliyopita WBA iliikataa Ofa ya kwanza kumnunua Berahino mwenye Miaka 22 huku Mwenyekiti wa WBA, Jeremy Peace, akidai hawana Ajenda ya kumuuza.
Hata hivyo, Berahino aliondolewa Kikosini na Meneja Tony Pulis wakati WBA inacheza na kufungwa 3-2 na Chelsea Jumapili kwa madai kuwa akili yake haijatulia.
Berahino, ambae amechipukia tangu utotoni hapo WBA na pia kuzichezea kwa Mkopo Klabu za Northampton, Brentford na Peterborough, ameichezea WBA Mechi 83 na kufunga Bao 29.
Kwa ajili ya Msimu huu mpya, WBA tayari imeshasaini Mastraika wengine wapya Rickie Lambert toka Liverpool na Salomon Rondon kutoka Zenit St Petersburg ya Urusi kwa Dau la Pauni Milioni 12 ambayo ni rekodi kwa Klabu hiyo.
JOHN STONES-KWENDA CHELSEA, SHIDA!
Baada ya Chelsea kugomewa Ofa zao mfululizo za kumnunua Beki wa Everton John Stones, Mchezaji huyo sasa ameamua mwenyewe kulazimisha Uhamisho wake kwa kuandika Barua rasmi kutaka ahame.
Tayari Chelsea washatoa Ofa za Pauni Milioni 20 na zikafuata za Milioni 26 na 30 kwa ajili ya kumnunua Stones mwenye Miaka 21 na zote kugomewa na Everton.
Stones kwa sasa ni Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya England na alinunuliwa na Everton Februari 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 3 kutoka Barnsley
 
FULU VIWANJA