Social Icons

Pages

Tuesday, 21 April 2015

Stori mpya kuhusu Jurgen Klopp kutua Arsenal


Klopp-Wenger
KUFUATIA kuanza vibaya msimu huu, mashabiki wa Arsenal walipoteza imani juu ya kocha wao, Arsene Wenger, lakini sasa wamerudisha imani yao kutokana na matokeo wanayoendelea kupatikana.
Kocha huyo mkongwe aliyejiunga na Arsenal mwaka 1996 kwasasa inaonekana kuwa na  uhakika wa kazi yake Emirates, lakini gazeti la Ujerumnai la Kickerlimeripoti stori ya kuvutia leo hii.
Jurgen Klopp siku za karibuni ametangaza kuondoka Borussia Dortmund naKickerlimedai kuwa Klopp ana nafasi kubwa ya kumrithi Arsene Wenger majira ya kiangazi mwakani.
Pia Klopp mwenye miaka 47 anahusishwa kujiunga na klabu za Liverpool na Manchester City.
Mwandishi wa Kicker ameripoti kwamba Arsene Wenger anaweza kupewa majukumu mengine katika klabu hiyo huku Jurgen Klopp akikabidhiwa nafasi ya kocha mkuu.
Arsenal wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe la FA kwa mwaka wa pili mfululizo na pia wanapambana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao na mpaka sasa unaweza kusema wana uhakika.
 
FULU VIWANJA