Social Icons

Pages

Sunday, 8 February 2015

VPL: SUPASTRAIKA MRISHO NGASSA AIPANDISHA YANGA KILELENI, ‘ AIUA ’MTIBWA

STRAIKA mahiri wa Yanga,
Mrisho Ngassa, Leo hii ndani
ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam alifunga Bao 2 na
kuipa ushindi Yanga wa Bao
2 -0 walipoilaza Mtibwa Sugar
kwenye Mechi pekee ya Ligi
Kuu Vodacom .

Hadi Mapumziko, ngoma
ilikuwa Droo 0 - 0.

Kipindi cha Pili , Dakika za 56
na 63, Mrisho Ngassa, ambae
alianzia Benchi kwenye Mechi
hii na kuingizwa Kipindi cha
Pili kuchukua nafasi ya Straika
kutoka Liberia Khpar Sherman ,
aliwapa furaha Washabiki wa
Yanga kwa kupachika Mabao
ambayo yamewafanya
wawatambuke Mabingwa
Watetezi Azam FC na kutwaa
tena uongozi wa Ligi Kuu
Vodacom .

Baada ya Mechi 13, Yanga
wana Pointi 25 wakifuatiwa na
Azam FC wenye Pointi 22 kwa
Mechi 12

Ligi itaendelea Jumatano
Februari 11 kwa Mechi 3
ambapo Azam FC watacheza na
Mtibwa Sugar huko Azam
Complex Jijini Dar es Salaam
wakati Yanga pia watakuwa
Jijini Dar es Salaam Uwanja
wa Taifa kucheza na Ndanda
FC huku huko Tanga Mgambo
JKT watacheza na Simba .

 
FULU VIWANJA