Social Icons

Pages

Sunday, 8 February 2015

MOURINHO: ‘ KUONGOZA POINTI 7 SI KITU !’ , PELLEGRINI ALIA KUKOSA UBUNIFU , WENGER AJUTIA MAKOSA YAO!


BAADA ya Jana Chelsea
kuzidisha pengo lao la
kuongoza Ligi Kuu England
kufikia Pointi 7 kufuatia wao
kushinda na Mabingwa
Watetezi Manchester City
kutoka Sare huku Arsenal
wakiendelea kutupwa mbali
baada ya kuchapwa na
Tottenham kwenye Dabi ya
London ya Kaskazini,
Mameneja wa Timu hizo 3
waliongea
.
PATA NINI WALICHOKISEMA:

MANUEL PELLEGRINI: MAN
CITY INAKOSA UBUNIFU!
Bosi wa Manchester City
Manuel Pellegrini amesema
Timu yake inakosa ubunifu
mara baada ya Jumamosi
kunusurika kufungwa na Hull
City baada ya Frikiki ya Dakika
za Majeruhi ya James Milner
kuwapa Sare ya 1 -1 .

Hull City, Timu ambayo iko
nafasi ya tatu toka mkiani mwa
Ligi Kuu England, iliongoza kwa
Bao la Dakika ya 35 la David
Meyler .

Hivi sasa City wameshacheza
Mechi 4 za Ligi bila ushindi na
wapo Nafasi ya Pili wakiwa
Pointi 7 nyuma ya Vinara
Chelsea.

Pellegrini aliongea:
“ Tunajaribu mno lakini
tunakosa ubunifu … . Timu
imetulia na ina ari lakini
imekosa Wachezaji wabunifu
wa kutengeneza nafasi dhidi ya
Timu kama Hull zinazojilinda
kikamilifu!”

City imemkosa Kiungo wao
mahiri Yaya Toure, ambae
yuko na Nchi yake Ivory Coast
kwenye AFCON 2015 huko
Equatorial Guinea , na tangu
Januari 4 walipoifunga
Sheffield Wednesday kwenye
Raundi ya 3 ya FA CUP
hawajashinda tena.

JOSE MOURINHO: ‘ KUONGOZA
POINTI 7 SI KITU!’
Jose Mourinho anaamini
kuongoza kwa Pointi 7 kwenye
Ligi Kuu England si kitu
kikubwa sana.

Akiongea baada ya kuifunga
Aston Villa hapo Jumamosi Bao
2 -1 huko Villa Park , Mourinho
alisema: “ Kwa Nchi nyingine
ningesema ni jambo safi sana .

Lakini kwa Nchi hii sio kitu.
Bado kuna Gemu 14 kumaliza
Ligi na zipo Pointi 42 za
kugombewa. Kila Gemu ni
ngumu na lolote linaweza
kutokea!”

Mourinho alisisitiza
hakustushwa na City kutoka
Sare na Hull City ambayo iko
chini kwenye Ligi ingawa
anafurahishwa kwamba
matumaini yao ya kuwa
Mabingwa yako mikononi
mwao wenyewe.

Amesema: “ Sishangazwi na
chochote hapa ! Nchini hapa
Timu yoyote inaweza kuzoa
Pointi!”

WENGER AJUTIA MAKOSA
YAO!
Bosi wa Arsenal Arsene
Wenger amekubali Timu yake
ilifanya makosa mengi wakati
Jumamosi ilipofungwa Bao 2- 1
na Tottenham kwenye Dabi ya
London Kaskazini .

Arsenal walitangulia kufunga
kwa Bao la Mesut Ozil lakini
Spurs wakapata ushindi huku
Bao zote zikifungwa na Harry
Kane .

Wenger amekiri matatizo ya
kiufundi kwenye Kiungo na
Difensi yao ndio
yaliwaangusha.

Jumanne Arsenal wanarudi
dimbani wakiwa kwao
Emirates kucheza na Timu ya
mkiani Leicester City huku
akitegemea Mfungaji wao
mkuu , Alexis Sanchez , atarejea
kilingeni baada ya kupona
tatizo la Musuli za Pajani .

 
FULU VIWANJA