VIGOGO wa England,
Manchester United, ambao wao
pamoja na Mabingwa Watetezi
Arsenal, ndio wanashika
Rekodi ya kutwaa FA CUP mara
nyingi, mara 11 kila mmoja ,
Jumanne Usiku wanarudiana
na Cambridge United Uwanjani
Old Trafford baada ya kutoka
0 -0 katika Mechi ya kwanza
iliyochezwa Abbey Stadium
Nyumbani kwa Timu hiyo ya
Daraja la Chini , Ligi 2 .
Hii ni Mechi ya Raundi ya 4 ya
FA CUP na Mshindi atatinga
Raundi ya 5 na kucheza na
Mshindi kati ya Preston au
Sheffield United ambao nao
wanarudiana Jumanne .
Mara ya mwisho na pekee kwa
Cambridge United kucheza
Uwanjani Old Trafford ni
Mwaka 1991 walipotwangwa
Bao 3 - 0 kwenye Kombe la Ligi
ambalo sasa linaitwa Capital
One Cup.