Matumaini ya wapenzi na mashabiki
wa Simba yamerudi baada ya
kuibuka na ushindi wa bao 2-0
wakiwafunga Polisi Morogoro katika
mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara
uwanja wa Jamhuri mkoani
Morogoro.
Goli la kwanza la Simba lilifungwa
dakika ya 14 ya mchezo kupitia kwa
Ibrahim Hajib ambaye aliunganisha
pasi ya Juko Murshid na kufanya
mchezo huo kwenda mapumziko
Simba wakiongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Simba ilipata pigo
baada ya kipa wake namba moja Ivo
Mapunda kuumia na kupelekwa moja
kwa moja katika hospital ya mkoa
wa Morogoro.
Simba ikapata bao la pili kupitia kwa
Elias Maguri akitumia makosa ya
kipa wa Polisi aliyetoka langoni bila
mipango.
Kwa matokeo hayo Simba imepanda
mpaka nafasi ya 3 ikiwa na pointi 20
pointi 5 nyuma ya Azam na Yanga
MATOKEO MENGINE
Kagera Sugar 1-0 JKT Ruvu