Kocha wa Mwadui Jamuhuri Kiwelu
maarufu kama Julio leo
amekiongoza kikosi cha Mwadui FC
kupanda daraja kwa kuichapa
Burkinafaso FC kwa bao 4-3
Julio ambaye msimu uliopita
alikaribia kurudi ligi kuu akiwa na
timu hiyo amekomaa mpaka kupata
nafasi moja kati ya 4 ambazo zilikua
zikigombaniwa.
Pamoja na Mwadui timu zingine
zilizopata nafasi ya kupanda ligi kuu
zikitokea ligi daraja la kwanza ni
pamoja na Toto Africans ya Mwanza,
Majimaji ya Songea na Afrikan
Sports ya Tanga.