BAADA ya Timu yake
kubandikwa 4- 0 Jumamosi
Uwanjani Vicente Calderón na
Mahasimu wao wakubwa
Atletico Madrid , Cristiano
Ronaldo amesema hiyo ni Siku
inayopaswa kusahaulika
haraka huku pia akikiri Real
Madrid ilikosa ari , nia na
utayari wa kiakili na kimwili.
Ronaldo, ambae ndie Mchezaji
Bora Duniani kwa Miaka Miwili
mfululizo hivi sasa, amesema:
“ Tulicheza vibaya sana katika
kila idara , kila sehemu. Ni Siku
inayopaswa kusahauliwa
haraka mno kwani Real Madrid
haiwezi kufungwa na Timu
yeyote Duniani Bao 4- 0 !”
Ronaldo alikiri kuwa Timu yao
ilikosa ari na haikuwa na
mwelekeo wowote: “Timu
haikuwa na utayari wa kiakili
na kimwili!”
Hata hivyo Ronaldo alisisitiza
wao bado wanaongoza Ligi na
ni muhimu watilie mkazo
Mechi zijazo.
Lakini pia Ronaldo alikiri kuwa
sasa Dabi za Jijini Madrid , El
Derbi Madrileno , zimebadilika .
Alieleza: “ Ni ukweli . Katika
Mechi za hivi karibuni
tumeshindwa kuwafunga
Atletico.
Mpaka Miaka Miwili
iliyopita, Atletico ilishindwa
kuifunga Real kwa Miaka 18 au
20. Lazima turudie ile Real
Madrid ya enzi, tunaweza
kuwafunga wao, licha ya kuwa
wazuri .”
Hata hivyo , Ronaldo alisisitiza
kuwa watatwaa Ubingwa wa La
Liga Msimu huu .