JANA USIKU huko Estadio de
Bata, Mjini Bata Nchini
Equatorial Guinea , Ivory Coast
waliibuka Bingwa wa Mataifa
ya Afrika kwenye Mechi ya
Fainali ya Kombe la Mataifa ya
Afrika, AFCON 2015 ,
walipoibwaga Ghana kwa
Mikwaju ya Penati 9 - 8 kama
walivyofanya Mwaka 1992.
Hii ni mara ya pili kwa Ivory
Coast kutwaa Ubingwa wa
Afrika na mara ya kwanza ni
Mwaka 1992 walipoitoa Ghana
pia kwa Mikwaju ya Penati
11- 10 baada ya suluhu ya 0 -0 .
Hii pia ni mara ya pili kwa
Kocha wa Ivory Coast, Herve
Renard , kutwaa Ubingwa wa
Afrika na mara ya kwanza
ilikuwa 2012 alipoiwezesha
Zambia kutwaa Ubingwa, tena
kwa kuifunga Ivory Coast, na
sasa kuweka Rekodi ya kuwa
Mtu wa kwanza kutwaa
Ubingwa wa Afrika na Nchi
mbili tofauti .
Hapo Jana Shujaa wa Ivory
Coast ni Kipa wao Boubacar
Barry ambae aliokoa na pia
kufunga Penati muhimu
iliyowapa Ivory Coast
Ubingwa .
Kila Timu ilikosa Penati 5 na
ndipo Kipa Barry akaokoa
Penati iliyopigwa na Kipa
mwenzake Brimah Razak na
kisha kufunga Penati ya
ushindi .
Kwa Kocha wa Ghana , Avram
Grant , hii ni mara ya pili
kushindwa Fainali kubwa kwa
Mikwaju ya Penati baada ya
Mwaka 2008 , akiwa na
Chelsea, alipobwagwa kwa
Mikwaju ya Penati na
Manchester United kwenye
Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI huko Moscow , Urusi .
Ghana, ambao mara ya mwisho
kati ya mara zao 4 kuwa
Bingwa wa Afrika ilikuwa 1982 ,
wangeweza kushinda Fainali
hii hasa baada ya kupata nafasi
kadhaa katika Dakika 120 za
Mchezo na mara mbili kupiga
Posti .
Pia hata kwenye Mikwaju ya
Penati walianza kwa mguu
mzuri pale Ivory Coast
walipokosa Penati zao 2 za
kwanza kwa Mchezaji mpya
wa Manchester City, Wilfried
Bony , kupiga Posti na Junior
Tallo kutoa nje lakini Ghana
nao , kupitia Afriyie Acquah na
Frank Acheampong , wakakosa.
Baada ya Wachezaji wote wa
ndani kumaliza kupiga Penati
zao ikaja zamu za Makipa na
ndipo Kipa Boubacar Barry
akaokoa Penati iliyopigwa na
Kipa mwenzake Brimah Razak
na kisha kufunga Penati ya
ushindi kwa Ivory Coast
kutwaa Ubingwa kwa Penati
9 -8 .