Social Icons

Pages

Tuesday, 17 February 2015

MESSI AMKIMBIZA RONALDO KIMYA KIMYA


Balaa la Lionel Messi liliendelea
juzi usiku wakati alipoiongoza timu
yake ya Barcelona kuibuka na
ushindi mnono wa bao 5-0
wakiifunga Levante katika mfululizo
wa Mechi za La Liga

Lionel Messi alifunga hat trick yake
ya 23 katika mchezo wa 300 katika
La Liga na kumfanya kufikisha
magoli 26 msimu huu magoli mawili
nyuma ya Ronaldo anayeongoza.

Messi amefikia rekodi ya Ronaldo ya
kufunga Hat trick nyingi zaidi katika
la liga wote wawili wakiwa sawa
mara 23.

Ushindi huo umeifanya Barcelona
kuitishia nyau Real Madrid ambao
wanaongoza ligi hiyo tofauti ikiwa ni
pointi moja tu hivi sasa.

Messi alifunga mabao matatu peke
yake huku Neymar na Suarez
wakifunga bao moja moja na Neymar
kufikisha bao la 17 msimu huu
katika ligi kukamilisha ushindi huo
wa bao 5-0.

Ushindi wa Jana kwa Barcelona
unawafsnya kufikisha michezo 11
bila kufungwa katika mashindano
yote wakifikia rekodi waliyoiweka
msimu wa mwaka 2008/2009
wakiwa chini ya kocha Pep
Guadiola.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique
akizungumzia rekodi ya kushinda
michezo 11 mfululizo alisema
"Rekodi ni nzuri lakini hazinivutii
mimi kwani haijalishi ni mechi ngapi
tumeshinda lakini kinacholeta maana
ni kujua vipi ushindi huo
umetusaidia kushinda makombe"

 
FULU VIWANJA