Social Icons

Pages

Tuesday, 17 February 2015

HIZI NDIZO TAMBO ZA YANGA BAADA YA KUFIKA MBEYA

Dar es Salaam
Baada ya kuwachapa ‘Makhrikhri’ BDF
XI FC ya Botswana, kikosi cha Yanga
SC tayari kimo jijini Mbeya kusaka
pointi sita za Ligi Kuu Tanzania Bara
kabla ya kuwafuata maafande wa BDF
XI FC mjini Gaborone, Botswana.
Wakiwa jijini Mbeya jioni hiui, Yanga
SC wametamba kuchukua pointi zote
sita katika mechi mbili za Ligi Kuu
jijini humo dhidi ya timu ‘kibonde
msimu huu’, Tanzania Prisons na
Mbeya City FC.

Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari
na Mawasiliano ya Yanga SC,
ameuambia mtandao huu muda mfupi
uliopita kuwa wachezaji wametua
jijini Mbeya salama wakitokea jijini
hapa.

Muro, mwandishi bora wa habari
nchini miaka minne iliyopita,
wachezaji wametinga jijini Mbeya kwa
mafungu, baadhi wakisafiri kwa ndege
na wasiopenda usafiri huo wa anga
wamesafirishwa kwa basi.

“Tumeingia Mbeya kwa malengo
mawili; kwanza kuchukua pointi zote
sita katika mechi mbili zijazo dhidi ya
Prisons na Mbeya City ili tukae vizuri
katika msimamo wa Ligi Kuu. Pili,
kufanya maandalizi ya mechi ya
marudiano na BDF XI FC nchini
Botswana,” amesema Muro.

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu
Tanzania Bara, Alhamisi Yanga SC
itashuka Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine mjini Mbeya kuwakabili
Prisons kabla ya kuchuana na wababe
wa Simba SC, Mbeya City FC kwenye
uwanja huo Jumapili.

Baada ya mechi dhidi ya City FC,
Yanga SC wataanza safari kuelekea
mjini Gaborone, Botswana kwa ajili ya
mechi yao ya marudiano dhidi ya
‘Makhrikhri’ BDF XI FC ya hatua ya
awali ya Kombe la Shirikisho barani
Afrika Februari 27.

Kikosi cha Mdachi Hans van der
Pluijm cha Yanga SC kiliinyuka timu
hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana
mabao 2-0 katika mechi ya kwanza
Uwanja wa Taifa jijini hapa juzi
(Jumamosi).

Shukrani kwa mabao ya mfungaji bora
wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu
uliopita, Mrundi Amisi Tambwe, yote
akiyafunga kwa vichwa na kufikisha
mabao manne katika mashindano yote
msimu huu.

Wachezaji wawili, kiungo Nizar
Khalfan na beki wa kati Pato
Ngonyani, ambao wamebaki jijini hapa
kutokana na maradhi.

Yanga SC kwa sasa inakamata nafasi
ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara ikiwa na pointi 25,
sawa na mabingwa Azam FC ambao
wako kileleni mwa msimamo kwa
faida ya tofauti nzuri ya mabao ya
kutupia na kufungwa.

Azam FC inayonolewa na Mcameroon
Joseph Omog, imefunga mabao 22 na
kufungwa 12 wakati Yanga SC
imetikisa nyavu za wapinzani mara 15
huku safu yake ya ulinzi
inayoongozwa na Nahodha, Mzanzibar
Nadir ‘Cannavaro’ imeruhusu mabao
saba.
By Na Bertha Lumala,

 
FULU VIWANJA