Social Icons

Pages

Tuesday, 17 February 2015

CANNAVARO ASEMA NGASSA YUPO VIZURI.


NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ ametamka kuwa
mshambuliaji wa kikosi hicho,
Mrisho Ngassa yupo vizuri kauli
iliyoungwa mkono na kocha
Mholanzi, Hans Pluijm, ambaye
huwa hana kawaida ya kumsifia
mchezaji mmoja mmoja.

Lakini kwa Cannavaro, ameshindwa
kuvumilia na kumsifia mshambuliaji
huyo ambaye tangu msimu mpya
ulipoanza alidaiwa amekwisha
makali.

Pluijm alisema anafurahishwa na
Ngassa namna anavyokuwa
kiunganishi mzuri katika safu ya
ushambuliaji kiasi cha kuwa chachu
ya ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi
ya BDF ya Botswana kwenye Kombe
la Shirikisho Jumamosi iliyopita.

“Ngassa yuko vizuri alifanya vile
nilivyotaka, alikuwa anahama
upande mmoja hadi mwingine,
alicheza kwa nafasi na malengo
akawa kiunganishi mzuri wa safu ya
ushambuliaji, nilipenda,” alisema
Pluijm na kufafanua sababu ya
kumtoa Tambwe na kumwingiza
Kpah Sherman ni kuwa alishindwa
kujiachia akawa anasimama sehemu
moja.

Cannavaro naye aliliambia
Mwanaspoti akisema: “Bado
hatujawa vizuri sana kwenye
ushambuliaji lakini kidogo mambo
mazuri na kama ulivyoona namna
Ngassa alivyokuwa vizuri. Kijana
ameibuka, naweza kusema
nimependa sana alivyocheza
kwenye mechi yetu na BDF.”

Mbali na hao, Kocha mkuu wa BDF,
Letang Kgengwenyane alisema,
mchezaji aliyekuwa amevaa namba
17 ambaye ni Ngassa ni mzuri sana
na ndiyo alikuwa tishio walipocheza
nao.

“Yanga ina wachezaji wazuri lakini
nimempenda sana yule aliyekuwa
amevaa namba 17 (Ngassa) alijua
majukumu yake na alitusumbua
sana,”alisema Kgengwenyane.
Naye Ngassa alisema: “Mazoezi
ndiyo siri, awali sikuwa vizuri kwa
sababu mbalimbali, lakini sasa
nataka kuwafanyia kitu Yanga.”

Kufanya vizuri kwa Ngassa ni kama
anaibuka upya, kwani tangu
ulipoanza msimu makali yake
yalipungua lakini aliibuka
walipocheza na Mtibwa Sugar
alipofunga mara mbili.

by mwanaspoti..

 
FULU VIWANJA