MABINGWA wa Tanzania Bara,
Azam FC , Leo wameanza
vyema kampeni yao katika
Mashindano ya CAF
CHAMPIONZ LiGI walipoichapa
El Merreikh ya Sudan Bao 2 -0
katika Mechi ya Raundi ya
Awali iliyochezwa Azam
Complex , Chamazi ambavyo ni
Viunga vya Jiji la Dar es
Salaam.
Azam FC wamefuata nyayo za
Yanga ambao hapo Jana
kwenye Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es Salaam waliichapa
Klabu ya Botswana BDF XI Bao
2 -0 katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Awali ya
Mashindano ya CAF ya Kombe
la Shirikisho .