LEO USIKU huko Deepdale,
Wenyeji Preston North End ,
Timu ya Daraja la chini Ligi 1 ,
watacheza na miamba ya Soka
ya England Manchester United
katika Mechi ya mwisho ya
Raundi ya 5 ya FA CUP
kuwania nafasi moja iliyobaki
kutinga Robo Fainali .
Preston North End
wanaongozwa na Simon
Grayson ambae Mwaka 2010
aliiongoza Leeds United
kuibwaga Man United nje ya FA
CUP kwa Bao 1 - 0 Uwanjani Old
Trafford kwa Bao la Jermaine
Beckford ambae sasa ni
Mchezaji wa Preston lakini
ataikosa Mechi hii kwa kuwa ni
mgonjwa .
Lakini Preston wanaweza
kumtumia Mkongwe wa Miaka
38, Kevin Davies , ambae ni
Straika wa zamani wa Bolton
Wanderers mwenye Rekodi ya
kuwa na Kadi nyingi katika
Historia ya Ligi Kuu England
ambae ana Historia ndefu ya
kukwaruzana na Man United
kila wanapokutana .
Mwaka 2007 huko Reebok
Stadium Davies alimchezea
Rafu mbaya Patrice Evra kiasi
cha Sir Alex Ferguson
kupandwa jazba kwenye
Benchi na hasira hizo
zilipozwa na Refa Mark
Clattenburg kumpa Kadi
Nyekundu Davies.
Inadaiwa baada ya tukio hilo
Evra alimuuliza Davies
kwanini Siku zote wakikutana
humuumiza na Davies kujibu :
“ Kwa sababu sikupendi !”