Leo Mabingwa Watetezi wa
Bundesliga , Bayern Munich
wakiwa kwao Allianz Arena
wameitandika Hamburger SV
Bao 8 - 0 katika Mechi ya
Bundesliga .
Bao za Bayern zilifungwa na
Thomas Muller, Bao 2 moja
kwa Penati, Arjen Robben , Bao
2 , Mario Götze, Bao 2, wakati
Franck Ribbery na Robert
Lewandoeski walifunga Bao 1
kila mmoja .
Nayo Timu ya Pili , VfL
Wolfsburg, wakicheza Ugenini,
waliichapa Bayer 04
Leverkusen Bao 5 -4 huku
Wachezaji wao Bas Dost
akipiga Bao 4 na Naldo
akifunga moja wakati Bao za
Leverkusen zilifungwa na Son
Heung- Min, Bao 3 , na Bellarabi
K . Bao 1 .
Matokeo haya yamewabakisha
Bayern Munich kuongoza Ligi
wakiwa Pointi 8 mbele ya VfL
Wolfsburg.