LIGI KUU VODACOM
imeendelea Leo kwa Mechi
kadhaa na Mabingwa Watetezi
Azam FC kushinda huko
Shinyanga na kutwaa uongozi
wa Ligi toka kwa Mtibwa Sugar
ambao wanacheza Kesho
Jumapili huku Yanga
wakiteleza kutwaa uongozi huo
baada ya kubanwa kwa Sare ya
0 -0 Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam.
Yanga, wakicheza na Ruvu
Shooting , walistahili ushindi
lakini walishindwa kufunga
wakati walipata nafasi za wazi
kibao .
Huko Kambarage, Shinyanga,
Azam FC wameifunga Stand
United Bao 1 -0 kwa Bao la
Dakika ya 43 la Frank Domayo
na kukaa kileleni mwa Ligi
wakiwa Pointi 1 mbele ya
Mtibwa Sugar ambao
wanacheza Jumapili Ugenini
na JKT Ruvu .
Huko CCM Kirumba, Mwanza ,
Mbeya City wameifunga Kagera
Sugar, wanaotumia Uwanja huo
kwa Mechi za Nyumbani baada
Kaitaba kufungwa kwa
ukarabati, Bao 1 -0 kwa Bao la
Dakika ya 80 la Peter
Mapunda .
Nao Simba wameichapa
Ndanda FC waliokuwa kwao
Uwanja Nangwanda Bao 2 -0
kwa Bao za Dan Sserunkuma
na Elias Maguri.
RATIBA
Jumapili Januari 18
JKT Ruvu v Mtibwa Sugar
Coastal Union v Polisi
Morogoro