SWANSEA 0 CHELSEA 5
Chelsea, wakicheza Ugenini,
wamepaa kileleni mwa Ligi Kuu
England wakiwa Pointi 5 mbele
ya Mabingwa Watetezi Man
City baada ya kuitandika
Swansea City Bao 5 -0 .
Chelsea walipata Bao lao la
kwanza Sekunde 50 tu tangu
Gemu ianze kupitia Oscar,
kisha Diego Costa akapiga Bao
2 na Oscar kuongeza jingine na
kuifanya Chelsea iwe 4 -0 hadi
Mapumziko.
Kipindi cha Pili , Andre Schurrle
akaipa Chelsea Bao la 5
kuiacha Swansea wawe bila
ushindi katika Mechi zao 4 za
QPR 0 MAN UNITED 2
Bao 2 za Kipindi cha Pili za
Marouane Fellaini na James
Wilson zimewapa ushindi wa
Bao 2 - 0 Manchester United
waliocheza Ugenini Loftus
Road na QPR.
Ushindi huu umeifanya Man
United warudi Nafasi ya 3 na
kuitambuka Southampton
ambao baadae Leo wako
Ugenini kucheza na Newcastle .