MTIBWA SUGAR wamerudi
kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom
baada ya kutoka Sare 1 -1 na
JKT Ruvu katika Mechi
iliyochezwa Azam Complex
huko Chamazi kwenye Viunga
vya Jiji la Dar es Salaam.
JKT Ruvu walitangulia kupata
Bao Dakika ya 7 Mfungaji
akiwa Samuel Kamuntu na
Amer Ali kuisawazishia katika
Dakika ya 37.
Matokeo hayo yameifanya
Mtibwa Sugar kuing ’oa Azam
FC toka kileleni kwa kuikamata
kwa Pointi wote wakiwa na
Pointi 17 kwa Mechi 9 lakini
Mtibwa wana ubora wa Magoli.
Huko Mkwakwani Tanga,
Coastal Union ilibanwa na
kutoka Sare 0- 0 na Polisi
Morogoro matokeo ambayo
yamezipandisha Timu zote
kwa Polisi kukwea hadi Nafasi
ya 5 na Coastal kukamata
Nafasi ya 7 .
Ligi hii itaendelea hapo
Jumanne huko Mwanza kwa
Mabingwa Azam FC kuwavaa
Kagera Sugar ambao sasa
wanatumia CCM Kirumba kama
Uwanja wa Nyumbani baada ya
Kaitaba huko Bukoba kufungwa
kwa ukarabati.
RATIBA :
Jumanne Januari 20
Kagera Sugar na Azam FC
(Mwanza )
Jumamosi Januari 24
Azam FC v Simba
Kagera Sugar v Ndanda FC
Stand United v Coastal Union
Polisi Morogoro v Yanga
Mbeya City v Tanzania Prisons
Ruvu Shooting v Mtibwa Sugar
Januari 25.
JKT Ruvu v Mgambo JKT