Social Icons

Pages

Monday, 12 January 2015

USIKU HUU KUJULIKANA NANI ATACHUKUA TENA TUZO YA FIFA BALLON D'OR


HAFLA ya kumtangaza Mshindi
wa Tuzo ya Mchezaji Bora
Duniani kwa Mwaka 2014 , FIFA
2014 Ballon d' Or, itaanza Leo
Saa 2 na Nusu Usiku, Saa za
Bongo, kwenye Ukumbi wa
Kongresshaus Jijini Zurich
huko Uswisi .
Wagombea Watatu waliopigiwa
Kura , ambazo zilifungwa rasmi
hapo Novemba 21 , ni Cristiano
Ronaldo wa Klabu ya Real
Madrid , Manuel Neuer wa
Bayern Munich na Lionel Messi
wa Barcelona.
Hafla ya Tuzo ya FIFA ya
Mchezaji Bora Duniani
ilianzishwa Mwaka 1991 lakini
Mwaka 2010 iliunganishwa na
ile ya Jarida la France Football ,
Ballon d' Or, na kubatizwa FIFA
Ballon d' Or.
HII LEO:
Hafla :
FIFA Ballon d ’ Or
Mahali :
Kongresshaus , Zurich
(Switzerland )
Tarehe :
12 January 2015 kuanzia Saa 2
na Nusu Usiku
Tuzo zitakazotolewa:
FIFA Ballon d ’ Or
FIFA Tuzo ya Mchezaji Bora
wa Mwaka Mwanamke
FIFA Kocha Bora wa Mwaka
Wanaume
FIFA Kocha Bora wa Mwaka
Wanawake
FIFA Tuzo ya Rais [Presidential
Award]
FIFA Tuzo ya Uchezaji Haki
[Fair Play Award]
FIFA Tuzo ya Goli Bora la
Mwaka [ Puskas Award]
FIFA/ FIFPro World XI Kikosi
Bora cha Mwaka

 
FULU VIWANJA