Social Icons

Pages

Wednesday, 12 November 2014

HANS POPPE ASEMA MKUDE AMEAMUA KUBAKI SIMBA KUTOKANA NA KAULI YA MANJI



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ile kauli aliyowahi kuitoa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ndiyo imesababisha Yanga imkose kiungo Jonas Mkude.


Hans Poppe amesema kauli aliyowahi kuitoa Manji kuwa atawasajili wachezaji wa Yanga na kuwaacha wafanye mazoezi kwenye michanga ya ufukwe wa Coco Beach ndiyo imesababisha Mkude aone atapoteza kipaji chake.

“Huenda Yanga wangeweza kumpata huyu kijana, lakini sasa kama Manji alisema wachezaji wa Simba anaweza kuwasajili na kuwaacha wacheze mchangani ufukweni, Mkude akaona haitakuwa sawa.
“Hivyo ameamua kubaki nyumbani na sisi sasa tunaelekeza nguvu kwa kijana wetu Msuva, tutaandika barua ili Yanga watupe nafasi ya kuzungumza naye,” alisema Hans Poppe.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu alipinga kauli hiyo ya Hans Poppe akisema hawakuwahi kuwa na mpango wa kumsajili Mkude.

“Hatukuwahi kuwaza hivyo, hayo ni mambo ya magazeti,” alisema Beno.

Hata hivyo, taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza, kweli Yanga ilikuwa inammezea mate kiungo huyo lakini baada ya kuongezewa mkaaba wa miaka miwili na Simba, imeamua kuingia kwenye kale ka wimbo ka “Sizitaki mbicho hizi
 
FULU VIWANJA