Mechi ya Marudiano ya Nusu
Fainali ya Capital One Cup
Uwanjani Stamford Bridge kati
ya Chelsea na Liverpool ilienda
Dakika 120 baada ya kuwa
Sare 0 -0 katika Dakika 90 na
Chelsea kushinda Bao 1 -0
katika Dakika za Nyongeza 30.
Ingawa Chelsea walipata Sare
ya 1- 1 huko Anfield Wiki
iliyopita na kikawaida
wangeshinda kwa Goli la
Ugenini, Mashindano haya
hayahesabu Magoli ya Ugenini
kuwa Mawili hadi baada ya
Mechi kumaliza Dakika 120 .
Hata hivyo , Dakika ya 4 tu
baada ya Dakika za Nyongeza
30 kuanza , Frikiki ya Willian
iliunganishwa vizuri kwa
Kichwa na Baranislav Ivanovic
na kuwapa Chelsea Bao moja
na la ushindi .
Leo Jumatano ni Marudiano ya
Nusu Fainali nyingine kati ya
Sheffield United na Tottenham
Nyumbani kwa Sheffield .
Katika Mechi ya kwanza
iliyochezwa pia Wiki iliyopita
huko White Hart Lane,
Tottenham iliifunga Sheffield
United Bao 1 -0 kwa Bao la
Penati iliyotolewa Dakika ya
75 baada ya Jay McEveley
kuushika Mpira na Andros
Townsend kupiga Penati hiyo
na kufunga.