Social Icons

Pages

Monday, 19 January 2015

ARSENAL WAVUNJA UKIMYA NDANI ETIHAD

BAADA ya Miaka Mitano ya
kubamizwa huko Manchester
Leo hii Arsenal wametoka
kidedea baada ya kuwacharaza
Mabingwa wa England
Manchester City 2 -0 Uwanjani
Etihad Jijini Manchester na
wao kujiletea matumaini ya
kufuzu 4 Bora huku
wakiwaacha City wakiwa Pointi
5 nyuma ya Vinara Chelsea
kwenye Msimamo wa Ligi Kuu
England.

Ushindi huu umewafanya
Arsenal wawe Nafasi ya 5
wakiwa Pointi 1 nyuma ya Man
United walio Nafasi ya 4, Pointi
3 nyuma ya Timu ya 3
Southampton , Pointi 7 nyuma
ya City na Pointi 12 nyuma ya
Vinara Chelsea.

Kwa City hili ni pigo kubwa
hasa baada ya kuwa na wimbi
la Mechi 12 bila kufungwa na
hasa ukizingatia Mechi yao
inayofuata ya Ligi ni ya Ugenini
hapo Januari 31 huko Stamford
Bridge dhidi ya Chelsea .

Ushindi huu wa Arsenal
ulianza kwa Penati laini
aliyotoa Refa Mike Dean baada
ya kuamua Vincent Kompany
amemchezea Faulo Nacho
Monreal na Santi Cazorla
kufunga Penati hiyo katika
Dakika ya 24.

Arsenal walifunga Bao lao la
Pili Dakika ya 66 baada ya
Frikiki ya Cazorla
kuunganishwa kwa Kichwa na
Olivier Giroud .

 
FULU VIWANJA