Social Icons

Pages

Saturday, 31 January 2015

MPYA WA ARSENAL , PAULISTA, YUMO KIKOSINI KUCHEZA NA VILLA

BOSI wa Arsenal, Arsene
Wenger, amedokeza kuwa Beko
wao mpya kutoka Brazil
Gabriel Paulista ataanza
Benchi kwenye Mechi yao ya
Ligi Kuu England Uwanjani
Emirates watakapocheza na
Aston Villa hapo Jumapili .

Paulista, mwenye Miaka 24 ,
alikamilisha Uhamisho wake
kutoka Villareal ya Spain Wiki
hii kwenye Dili ambayo Straika
wa Arsenal, Joel Campbell,
alienda Villareal kwa Mkopo na
kuwagharimu Arsenal Pauni
Milioni 11. 5 .

Akimwelezea Paulista, Wenger
amesema Paulista mwenye
Urefu wa Futi 6 Inchi 2, ana ari
na umbo zuri la kufanikiwa
kucheza Soka la England na pia
ana uwezo wa kucheza Fulbeki
wa Kulia na Kushoto.

Wenger amesema : “ Gabriel
yuko tofauti na David Luiz
ambae ni rahisi kumchukulia
kama Kiungo Mkabaji badala
ya Sentahafu. Gabriel ni Beki
halisi. Yeye anatoka Sao Paolo.

Ni Paulista wa kweli . Huko
Brazil una Wachezaji wa Rio
na unao Wachezaji wa Sao
Paolo. Rio ni Bichi na Sao
Paolo ni Wachezaji wachapa
kazi!”

Hata hivyo , Paulista
hazungumzi neno hata moja la
Kiingereza na Kihispania chake
ni cha kubabaisha na Wenger,
ambae anazungumza Lugha
nyingi lakini si Kireno
anachoongea Paulista ,
amemtaka Mbrazil huyo
kuongeza juhudi ya kujifunza
Kiingereza .

Wenger ameeleza : “ Haongei
Kiingereza na hilo linaweza
kukufungisha. Anacheza nafasi
ambayo ni muhimu kujua
Kiingereza ili ashirikiane
vyema na wenzake. Tumeanza
kumfundisha maneno muhimu
kama vile ‘Ofsaidi ’ na
‘Mtazame Mshika Kibendera.

 
FULU VIWANJA