BAO la Dakika ya 89 la Alvaro
Morata limewapa Mabingwa
wa Italy Juventus ushindi wa
Bao 1 - 0 dhidi ya Parma
kwenye Mechi ya Robo Fainali
ya Coppa Italiana iliyochezwa
Stadio Tardini hapo Jana.
Kwenye Nusu Fainali, Juventus
watacheza na Mshindi kati ya
A SRroma na Fiorentina.
Mechi nyingine za Robo Fainali
zitapigwa Februari 3 kati ya AS
Roma na ACF Fiorentina na
Siku inayofuatia , ndani Stadio
San Paolo, Wenyeji SSC Napoli ,
ambao ndio Mabingwa
Watetezi wa Kombe hili ,
watakuwa kwao kucheza na
Inter Milan.
Kila Tmu tayari inajua nani
anaweza kuwa Mpinzani wake
endapo watafuzu kuingia Nusu
Fainali