Social Icons

Pages

Saturday, 31 January 2015

LEO KIMBEMBE: VINARA CHELSEA, BILA COSTA , KUWAVAA MAN CITY STAMFORD BRIDGE!

Vinara wa Ligi Kuu England ,
Chelsea, Leo wapo kwao
Stamford Bridge kucheza na
Mabingwa Watetezi
Manchester City na watacheza
Mechi hii bila ya Straika wao
Diego Costa ambae
amefungiwa Mechi 3 .

FA, Chama cha Soka England ,
Jana kilitangaza Adhabu ya
Kifungo cha Mechi 3 kwa Costa
kwa kosa la kumtimba
Mchezaji wa Liverpool, Emre
Can, Jumanne iliyopita wakati
wa Nusu Fainali ya Capital Oe
Cup

Adhabu hiyo itamfanya aikose
Mechi ya Leo na City pamoja
na zile dhidi ya Aston Villa na
Everton.

Chelsea, ambao wapo Pointi 5
mbele ya Man City walio
Nafasi ya Pili , huenda pia
wakamkosa Kiungo wao Cesc
Fabregas na Filipe Luis ambao
waliumia wakati wa Mechi na
Liverpool ya Capital One Cup.

City wao watamkosa Kiungo
wao Yaya Toure pamoja na
Mchezaji wao mpya Wilifred
Bony ambao wote wako huko
Nchini Equatorial Guinea
kuiwakilisha Nchi yao Ivory
Coast kwenye Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika,
AFCON 2015 .

 
FULU VIWANJA