KUNDI D la Mashindano ya
Mataifa ya Afrika, AFCON 2015,
limemaliza Mechi zao za
mwisho na Ivory Coast kutinga
Robo Fainali baada ya kuifunga
Cameroun lakini Mali na
Guinea zinangoja kurushwa
Shilingi kuamua nani
ataungana nao baada ya Timu
hizo kutoka Sare kwenye
Mechi yao ya mwisho na
kufungana kwa kila kitu.
IVORY COAST 1 CAMEROUN 0
>> Nuevo Estadio de Malabo ,
Mjini Malabo
Ivory Coast wametinga Robo
Fainali baada ya kuifunga
Cameroun Bao 1 -0 na kutwaa
uongozi wa Kundi D .
Ivory Coast walitinga Haftaimu
wakiwa Bao 1- 0 mbele kwa
Bao la Dakika ya 36 la Max -
Alain Gradel kwa Shuti la Mita
30.