CRISTIANO RONALDO, kwa Mwaka wa Pili mfululizo ameshinda FIFA Ballon d'Or ambayo ni Tuzo ya MchezajiBora Duniani kwa Mwaka 2014 na kuwafunika Wapinzake wake Lionel Messi na Manuel Neuer.Ronaldo alitangazwa Mshindi kwenye Hafla iliyofanyika Leo hii huko Ukumbi wa Kongresshaus Jijini Zurich huko Uswisi na hii ni mara ya 3 kwake kuizoa Tuzo hii ambayo Messi anaongoza kwa kuitwaa mara 4.Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Nadine Kessler wa Germany.Tuzo ya Goli Bora la Mwaka imeenda kwa Mchezaji mwenzake Ronaldo wa Klabu ya Real Madrid, James Rodriguez, kwa Goli lake aliloifungia Nchi yake Colombia ilipocheza na Uruguay.Kocha Bora wa Mwaka ni Joachim Low wa Mabingwawa Dunia Germany.Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Kipa Manuel Neuerwote pia walitajwa kwenye Listi ya Wachezaji 11 wa Kikosi Bora cha Mwaka, FIFA/FIFPro World XI, pamoja na Mabeki Phillip Lahm, David Luiz, Thiago Silva and Sergio Ramos, Viungo Andres Iniesta, Toni Kroos na Angel Di Maria pamoja na Fowadi Arjen Robben.Hafla ya Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani ilianzishwa Mwaka 1991 lakini Mwaka 2010 iliunganishwa na ile ya Jarida la France Football, Ballon d'Or, naTuzo zilizotolewa: FIFA Ballon d’Or==CristianoRonaldo FIFA Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Mwanamke==Nadine Kessler FIFA Kocha Bora wa Mwaka Wanaume==Joachim Low FIFA Kocha Bora wa Mwaka Wanawake==Ralf Kellermann FIFA Tuzo ya Rais [Presidential Award]==Hiroshi Kagawa FIFA Tuzo ya Uchezaji Haki [Fair Play Award]==Wanaojitolea FIFAFIFA Tuzo ya Goli Bora la Mwaka [Puskas Award]==Jame Rodriguez FIFA/FIFPro World XI Kikosi Bora cha Mwaka==-Kipa:Manuel Neuer (Germany/Bayern Munich), -Mabeki:Sergio Ramos (Spain/Real Madrid), David Luiz (Brazil/PSG), Philipp Lahm (Germany/Bayern Munich), Thiago Silva (Brazil/PSG), -Viungo:Andres Iniesta (Spain/Barcelona), Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina/Manchester United)-Mafowadi:Arjen Robben (Netherlands/Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina/Barcelona), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid).
WASHINDI WALIOPITA WA Ballon d'Or:
1956Stanley Matthews1957Alfredo Di Stefano1958Raymond Kopa1959Alfredo Di Stefano1960Luis Suarez1961Omar Sivori1962Josef Masopust1963Lev Yashin1964Denis Law1965Eusebio1966Bobby Charlton1967Florian Albert1968George Best1969Gianni Rivera1970Gerd Muller1971Johan Cruyff1972Franz Beckenbauer1973Johan Cruyff1974Johan Cruyff1975Oleg Blokhin1976Franz Beckenbauer1977Allan Simonsen1978Kevin Keegan1979Kevin Keegan1980Karl-Heinz Rummenigge1981Karl-Heinz Rummenigge1982Paolo Rossi1983Michel Platini1984Michel Platini1985Michel Platini1986Igor Belanov1987Ruud Gullit1988Marco van Basten1989Marco van Basten1990Lothar Matthaus1991Jean-Pierre Papin1992Marco van Basten1993Roberto Baggio1994Hristo Stoichkov1995George Weah1996Matthias Sammer1997Ronaldo1998Zinedine Zidane1999Rivldo2000Luis Figo2001Michael Owen2002Ronaldo2003Pavel Nedved2004Andriy Shevchenko2005Ronaldinho2006Fabio Cannavaro2007Kaka2008Cristiano Ronaldo2009Lionel Messi2010Lionel Messi2011Lionel Messi2012Lionel Messi2013Cristiano Ronaldo