Kipa
mkongwe Ivo Mapunda ambaye aliingizwa katika dakika ya 90 kuikoa Simba
kwenye mikwaju ya penalti wakati wa fainali za Kombe la Mapinduzi
anasema alijua lazima atapangua au kudaka angalau penalti moja.
Mapunda alisema wakati ameambiwa angie kuchukua nafasi ya Peter Manyika, alijua ana jukumu zito na aliapa angelitekeleza.
"Penalti
si kazi lahisi, ujuzi wa kipa lakini ujuzi wa mpigaji. Nilitaka angalau
nipangue mbili ikishindikana hata moja," alisema.
Kipa
huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa katika Ligi Kuu Kenya wakati
akiichezea Gor Mahia kutokana na upanguaji wa mikwaju ya penalti,
aliisaidia Simba kubeba ubingwa wa Mapinduzi baada ya kupangua penalti
ya Vicent Barnabas.