Alexis Sanchez ndiye bora kwa mujibu wa bosi wa Man City
Manuel
Pellegrini ameweka wazi mchezaji ambaye anaamini ni bora zaidi nchini
England…na cha kushangaza hajamtaja mshambuliaji wa Manchester
City,Sergio Aguero.
Kiukweli,
bosi huyo wa City aliweka wazi kuwa mchezaji bora wa EPL ni mkali wa
Arsenal, Alexis Sanchez ambaye alifunga na kutoa pasi ya mwisho katika
ushindi wa Gunners wa 3-0 dhidi ya Stoke City jumapili iliyopita.
Akizungumza
na AS, Mchile huyo mwenye miaka 61 alifafanua sababu inayomfanya aamini
kuwa nyota huyo ndiye bora kuwa ni kufunga magoli 12 na kutoa pasi za
mwisho 7 tangu asajiliwe kwa paundi milioni 32 kutoka Barcelona majira
ya kiangazi mwaka jana.