Social Icons

Pages

Monday, 26 January 2015

ARSENAL YAWAFUNDISHA TIMU KUBWA JINSI YA KUCHEZA NA TIMU NDOGO

Mabingwa watetezi wa kombe la FA
nchini England klabu ya Arsenal jana
ilizifundisha timu kubwa jinsi
ambavyo zinapaswa kucheza na
timu zilizo madaraja ya chini baada
ya kuifunga Brighton & Hove Albion
bao 3-2 katika mchezo uliopigwa
katika uwanja wa Brighton.

Arsenal ambao wanataka kutetea taji
hilo iliwachukua dakika 2 tu
kuandika bao safi kupitia kwa Theo
Walcot bao ambalo liliwachanganya
vilivyo Brighton ambao
wanafundishwa na kocha wa zamani
wa Newcastle Chris Hughton.

Badae Mesuit Oezil akafunga bao la
pili dakika ya 24 Ikiwa ni bao lake la
kwanza tangu atoke majeruhi kama
ilivyo kwa Theo Walcot ambaye
kabla ya bao la jana alikua hajafunga
tangu mwaka jana na goli la Tatu la
Arsenal lililofungwa na Tomas
Rosicky dakika ya 59
Brighton wao walipata magoli yao
kupitia kwa Chris O'Grady na Sam
Baldock.

Ushindi wa Arsenal umekua kama
fundisho kwa timu kubwa zote
ambazo zilishindws kupata ushindi
kwa timu za madaraja ya chini
nyingi zikitolewa huku Man United
na Liverpool itabidi wasubiri mpaka
mechi za marudiano kujua kama
watavuka kuingia robo fainali.

Ratiba ya michuano hiyo hatua
inayofata itapangwa leo wakati
kukiwa na mchezo wa mwisho leo
wa hatua ya 4 ambapo Rochdale
itaialika Stoke City katika mchezo
utakaoanza saa tano usiku.

 
FULU VIWANJA