Social Icons

Pages

Monday, 19 January 2015

CAPE VERDE WATOA SARE NA TUNISIA,LEO GHANA UWANJANI DHIDI YA SENEGAL

Huko Nchini Equatorial Guinea,
Mechi nyingine ya Kundi B la
Mashindano ya Mataifa ya
Afrika, AFCON 2015 , kati ya
Cape Verde na Tunisia
ilimalizika 1 -1 kama
ilivyokuwa kwa nyingine ya
Kundi hilo iliyochezwa
mapema Jana kwisha 1 -1 kati
ya Zambia na Congo DR .

Mechi zote hizo zilichezwa
Nuevo Estadio de Ebebiyín ,
Mjini Ebebiyin .

Kwenye Mechi ambayo kila
Timu ilikosa Mabao ya wazi,
Mohamed Ali Moncer aliipa
Tunisia Bao la kuongoza katika
Dakika ya 70 na Almeida
Heldon kusawazisha kwa
Penati Dakika 7 baadae .

Hii Leo zipo Mechi mbili za
Kundi C wakati Ghana
watacheza na Senegal huku
Algeria wakikwaana na South
Africa Mechi ambazo zote
zitachezwa Estadio de
Mongomo, Mjini Mongomo.

 
FULU VIWANJA